KENYATTA AMKABIDHI MADARAKA RUTO

Kenyatta amemkabidhi mamlaka kwa muda naibu wake William Ruto kwa siku mbili atakazokuwa nje.  Mahakama ya kimataifa ya ICC, inajiand...



Kenyatta amemkabidhi mamlaka kwa muda naibu wake William Ruto kwa siku mbili atakazokuwa nje. Mahakama ya kimataifa ya ICC, inajianda kuwa mwenyeji wa mkutano maalum wa siku mbili kuhusu kesi ya Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ambaye atakuwa rais wa kwanza aliye mamlakani kufika mbele ya mahakama hiyo.

Kenyatta anakabiliwa na tuhuma za uhalifu dhidi ya binadamu anazodaiwa kutenda baada ya uchaguzi wa mwaka 2007.Mahakama hiyo inasama kuwa Kenyatta alihusia katika kupanga na kufadhili ghasia za kikabila baada ya uchaguzi uliozua utata mwaka 2007/08Zaidi ya wakenya 1,000 waliuawa kwenye gasia hizo.


Ruto ambaye ni rais kwa muda naye pia anakabiliwa na kesi katika mahakama hiyo ya ICC
Mawakili wa Kenyatta wanasema kuwa kesi hiyo inapaswa kufutiliwa mbali kwa kukosa ushahidi.
Kenyatta ameombwa na mahakama hiyo kufika mbele yake ili kujadili malalamiko yaliyowasilishwa na kiongozi wa mashtaka Fatou Bensouda kwamba serikali ya Kenya imekataa kuwasilisha ushahidi unaohitajika katika kesi ya Kenyatta. 
Majaji wa mahakama hiyo hata hivyo watathmini kauli kutoka kwa pande zote mbili.

Mkutano huo wa siku mbili unatarajiwa pia kutangaza tarehe ya kuanza kusikilizwa kwa kesi dhidi ya Kenyatta.
ICC imemtaka Kenyatta kujibu madai ya upande wa mashitaka kuwa Kenya inakataa kutoa ushahidi unaotakikana na mahakama hiyo.


Rais Kenyatta akikagua gwaride la heshima kabla ya kuondoka nchini kuelekea Hague
Mwezi Septemba, mahakama iliahirisha kesi dhidi ya Kenyatta baada ya upande wa mashitaka kusema kuwa Kenya imekosa kutoa ushahidi unaotakikana na mahakama hiyo.

Mashahidi wa upande wa mashitaka wamejiondoa katika kesi hiyo.
Mamia ya wabunge wa Kenya wanatarajiwa kuambatana na Kenyatta kama ishara ya kumuunga mkono.
CHANZO BBC SWAHILI

Related

KOMBORA LALIPUA MATENKI YA MAFUTA

Vikosi vya zima moto vya Libya vinapambana kujaribu kuuzima moto baada ya kombora la roketi kulipua tanki la kuhifadhia mafuta wakati wa mapigano kati ya makundi mawili yanayohasimiana katika m...

LIVERPOOL YAMSAJILI DIVORC OROGI

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ubelgiji Divorc Origi hatimaye amejiunga na timu ya Liverpool. Baba yake Origi, Mike Okoth, ambaye ni mchezaji wa zamani wa timu taifa ya Kenya Harambee Stars ...

TAIFA STARS KUPIGA KAMBI MBEYA KUJIANDAA NA MSUMBIJI

Kikosi cha Taifa Stars kitapiga kambi ya wiki moja kujiandaa kwa mechi ya marudiano dhidi ya Msumbiji. Mechi hiyo ya raundi ya pili ya michuano ya Afrika kutafuta tiketi ya kushiriki Fainali za...

Post a Comment

emo-but-icon
:noprob:
:smile:
:shy:
:trope:
:sneered:
:happy:
:escort:
:rapt:
:love:
:heart:
:angry:
:hate:
:sad:
:sigh:
:disappointed:
:cry:
:fear:
:surprise:
:unbelieve:
:shit:
:like:
:dislike:
:clap:
:cuff:
:fist:
:ok:
:file:
:link:
:place:
:contact:


LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

904826
item