WATOTO 130000 WANAISHI NA MAAMBUKIZI YA VVU
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na watoto Dkt Pindi Chana. Dar Es Salaam TAKWIMU zinaonesha kwamba watoto 130000 wana ...
https://gabriellabridalsolution.blogspot.com/2014/11/watoto-130000-wanaishi-na-maambukizi-ya.html
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na watoto Dkt Pindi Chana.
Dar Es Salaam
TAKWIMU
zinaonesha kwamba watoto 130000 wana maambukizi ya Virusi Vya UKIMWI
(VVU) kati ya hao 39317 wamefikiwa na kupatiwa huduma ya dawa za
kupunguza makali ya virusi hivyo.
Hayo
yamesemwa leo na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto,
Dkt. Pindi Chana wakati akifungua kongamano la nne la kitaifa la VVU na
UKIMWI kwa watoto linalofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Kimataifa
wa Mwalimu Nyerere uliopo jijini Dar-es-salaam.
Dkt
. Chana alisema asilimia 39 ya watoto walio katika hatari ya kupata
maambukii ya UKIMWI hupimwa vipimo vya kubaini maambukizi ya VVU ndani
ya miezi miwili baada ya kuzaliwa hivyo basi kuna umuhimu kwa watoto
hawa kupata huduma za tiba mapema.
Akizungumzia
maambukizo ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto waziri huyo alisema
Tanzania imepiga hatua katika kuzuia maambukizo kutoka kwa mama kwenda
kwa mtoto lengo likiwa ni kutokomeza kabisa maambukizi mapya kwa watoto
wachanga.
“Mama
wajawazito na wale wanaonyoyesha wanapatiwa huduma ya dawa za kupunguza
makali ya VVU mara tu wanapogundulika kuwa na maambukizo, kupitia
mpango mpya unaojulikana kama ‘uwezekano namba 2 au (Option B+)”,
alisema Dkt.Chana
Alisema
kufikia mwezi Juni mwaka huu jumla ya akina mama 940900 kati ya
1050043 hii ni sawa na asilimia 89.6% ya waliohudhuria kliniki walipimwa
UKIMWI kati ya hao 47856 takribani asilimia 5 walikutwa na maambukizi
ya VVU.
Kwa upande wa watoto 20569 walipima kipimo cha DBS kati ya hao 2063 hii ni sawa na asilimia 10 walikutwa na maambukizo ya VVU.
Naye
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Donan Mbando,
alisema ingawa nchi imepiga hatua katika mapambano ya kudhibiti UKIMWI
hali halisi inaonyesha kuwa bado kuna maambukizo yanatokea sio tu kwa
watu wazima bali na kwa watoto pia.
“Ni
jukumu letu kuendelea kuweka mikakati ya dhati na kuisimamia ili
kuhakikisha lengo la kutokomeza maambukizo ya VVU tunalifikia kwani
mwaka 1986 maambukizi yalikuwa juu kwa asailimia 18 lakini hivi sasa
yameshuka na kufikia asilimia 5.3”, alisema Dkt. Mbando
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa ufundi kutoka Taasisi ya Elizabeth Glaser
Pediatric Aids (EGPAF) ambao ni waandaaji wa kongamano hilo Chrispin
Kimario alisema ni muhimu kwa wazazi na jamii kushirikiana kwa pamoja na
kulibeba jukumu la kuhakikisha kila mama mjamzito anapata huduma ya
vipimo husika na matibabu kwa wakati.
Kimario
alisema, “Watoto wameachwa nyuma, ni vyema tukumbuke kuwa mtoto
hawawezi kujipeleka wenyewe hospitali kupima afya zao, hivyo ni jukumu
letu wazazi, walezi na jamii kwa ujumla kuhakikisha watoto hawa wanapata
huduma wanazostahili”.
Kauli
mbiu ya kongamano hilo la siku mbili ambalo limehudhuriwa na wadau wa
afya kutoka asasi za umma na binafsi za ndani na nje ya nchi ni ongeza
kasi: Rahisisha upatikanaji wa utumiaji wa huduma za VVU na Ukimwi, pata
matokeo chanya ya afya za mama na watoto wanaoishi na VVU.