KITUO KIPYA CHA KUNUNULIA KARAFUU CHAFUNGULIWA RASMI

  Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Zanzibar, Mhe: Juma Duni Haji akiondoa kitambaa kuashiria kufungua kituo kipya cha kununulia kar...

 Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Zanzibar, Mhe: Juma Duni Haji akiondoa kitambaa kuashiria kufungua kituo kipya cha kununulia karafuu, kilichopo Kilindi wilaya ya Chake Chake Pemba, kilichojengwa na ZSTC, ikiwa ni shamra shamra ya kutimia miaka 51 ya mapinduzi Zanzibar.

 Baadhi ya wananchi wa shehia ya Kilindi wilaya ya Chake Chake Pemba, wakimsilikiza Mkurugenzi mtendaji wa ZSTC Zanzibar, Mwahija Al-masi Ali akizungumza kwenye ufunguzi wa kituo kipya cha kununulia karafuu kwenye shehia hiyo, ikiwa ni shamra shamra ya kutimia miaka 51 ya mapinduzi Zanzibar.

 Kikundi cha burudani cha Mkota ngoma cha Mkoani Pemba, kikitumbuiza kwa ngoma ya kibati, kwenye ufunguzi wa kituo kipya cha ununuzi wa karafuu shehia ya Kilindi wilaya ya Chake Chake Pemba, ikiwa ni shamra shamra ya kutimia miaka 51 ya mapinduzi ya Zanzibar.

Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Zanzibar, Mhe: Juma Duni Haji, akizungumza  na wananchi wa shehia ya Kilindi wilaya ya Chake Chake Pemba, mara baada ya kukifungua kituo kipya cha kununulia karafuu, kilichopo shehiani humo, ambacho kilijengwa na ZSTC, ikiwa ni shamra shamra ya kutimia miaka 51 ya mapinduzi Zanzibar.
 Picha zote na Haji Nassor, Pemba.
 

Related

OTHER NEWS 7897963837169638644

Post a Comment

emo-but-icon

FOLLOW US

.

LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

RECENT

Archive

item