MBUNGE GODFREY MGIMWA AKABIDHI MSAADA WA BATI KIJIJI CHA USENGERENDETI NA MAHANZI
Katibu wa mbunge wa jimbo la Kalenga Bw Martine Simangwa kushoto akikabidhi msaada wa bati 100 kwa uongozi wa kijiji cha Usen...
https://gabriellabridalsolution.blogspot.com/2014/07/mbunge-godfrey-mgimwa-akabidhi-msaada.html
Katibu wa mbunge wa jimbo la
Kalenga Bw Martine Simangwa kushoto akikabidhi msaada wa bati 100
kwa uongozi wa kijiji cha Usengerendeti kwa ajili ya ujenzi wa nyumba
ya wauguzi wa Zanahati ya kijiji .
Wananchi wakishiriki kushusha bati hizo
Katibu wa mbunge Mgimwa Bw
Martine Simangwa akieleza kazi mbali mbali zilizofanywa na mbunge
Godfrey Mgimwa toka alipochaguliwa
Katibu wa mbunge Mgimwa Bw
Martine Simangwa kushoto akikabidhi bati 80 kwa uongozi wa serikali
ya kijiji cha Mahanzi kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa
katika kijiji hicho kipya
Wananchi wakimpongeza katibu wa Mgimwa kwa niaba ya mbunge wao Godfrey Mgimwa
.............................................................................................
Na Francis Godwin Blog.
Na Francis Godwin Blog.
MBUNGE wa jimbo la Kalenga
Godfrey Mgimwa ametoa msaada wa bati 180 zenye tahamani ya zaidi ya
Tsh milioni 1 kwa kata ya Wasa kwa kama sehemu ya utekelezaji wa
ahadi zake katika kata hiyo.
Akikabidhi msaada huo kwa
niaba ya mbunge Mgimwa katibu wake Martine Simangwa alisema kuwa bati
hizo ni sehemu ya jitihada za mbunge huyo kuunga mkono harakati
za wananchi katika kuibua miradi ya kimaendeleo katika maeneo yao.
Hata hivyo alisema kuwa bati
hizo 100 ni kwa ajili ya kijiji cha Usengerendeti ambao wapo katika
ujenzi wa nyumba ya waganga katika Zahanati ya kijiji na bati 80
kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa shule katika kijiji kipya cha
Mahanzi .
Alisema kuwa moja kati ya
mambo ambayo mbunge Mgimwa ameyawekea kipaumbele zaidi ni pamoja na
elimu pamoja na afya na kuwa jitihada za kuhakikisha mambo hayo
yanashughulikiwa zinafanyika .
Pia alisema katika
kuhakikisha maendeleo ya jimbo hilo la Kalenga yanaendelea kusonga
mbele zaidi ni vema wananchi wa jimbo hilo kuelekeza nguvu zao
katika maendeleo na kuachana na baadhi ya watu wanaopita katika jimbo
hilo kwa ajili ya kuutaka ubunge mwaka 2015.
Kwani kufanya hivyo ni
kuendelea kurudisha nyuma maendeleo ya jimbo hilo na kuwataka
wanaofanya hivyo kwa sasa kusubiri muda ukifika ndipo wananze
kujipitisha na kuwa kimsingi katika nafasi ya ubunge hakuna mbunge
kivuli hivyo kitendo cha watu hao wanaojipitisha kufanya hivyo kwa
sasa ni kuvuruga kasi ya maendeleo ya jimbo hilo.
Akizungumzia kuhusu suala la
afya katika jimbo hilo alisema kuwa hali ya huduma ya afya bado si
mbaya sana japo kuna changamoto mbali mbali ambazo zinapaswa
kushughulikiwa ikiwemo ya dawa pamoja ,ukosefu wa nyumba za watumishi
wa afya na baadhi ya maeneo zahanati na vituo hivyo vya afya kukosa
umeme.
Awali wananchi wa kata hiyo
ya Wasa walimpongeza mbunge huyo kwa kuonyesha uaminifu kwao na
hata kuanza kutimiza ahadi zake kwa wakati mfupi zaidi
ukilinganisha na wabunge wengine waliopata kuongoza jimbo hilo
ambao hadi wameondoka madarakani baadhi ya ahadi hawajatekeleza kwa
wananchi.
Alisema Yohana Sanga kuwa
jimbo la Kalenga kwa muda mrefu limekuwa ni jimbo linaloongoza kwa
kubadili wabunge kwa kila kipindi kimoja na ndi sababu ya jimbo
hilo kuendelea kuwa nyuma katika maendeleo ukilinganisha na majimbo
ambayo wabunge wake wameongoza kwa zaidi ya kipindi kimoja na kuwa
kwa sasa wao hawana haja ya kubadili mbunge mwingine zaidi ya Mgimwa.