SEMA yatumia shilingi milioni 380 kusambaza Maji Iramba

  Mtendaji mkuu wa shirika la MEDICOR la nchini Uingereza, Fortunat Walther (wa kwanza kushoto) akitoa maelezo juu ya ujenzi wa visima v...

 Mtendaji mkuu wa shirika la MEDICOR la nchini Uingereza, Fortunat Walther (wa kwanza kushoto) akitoa maelezo juu ya ujenzi wa visima vya maji kwa meneja wa SEMA, Ivo Manyaku, wakati Walther alipotembelea miradi hiyo inayofadhiliwa na shirika lake.

Mtendaji mkuu wa shirika la MEDICOR la Uingereza, Fortunat Walther, akipiga picha ya jengo la kisima kilichojengwa wilayani Iramba.

Na Nathaniel Limu,  Iramba
SHIRIKA lisilokuwa la kiserikali Linaloboresha na Kusimamia Mazingira ili kuleta Maendeleo Endelevu (SEMA) la mjini Singida limetumia zaidi ya sh milioni 380 kwa ajili ya utekelezaji  mradi wa maji wilayani Iramba, mkoani Singida kati ya Julai 2013 na Machi mwaka huu.
Meneja wa Shirika la SEMA (Sustainable Environment Management Action), Ivo Manyaku, alisema kuwa mradi huo uliofadhiliwa na Shirika la WaterAid la jijini Dar es Salaam, umetekelezwa katika vijiji viwili vya Mgongo na Kisunga-Shelui pamoja na kitongoji cha Kibululu wilayani humo.
Manyaku alisema kuwa mradi huo umelenga kufaidisha jumla ya wakazi 7,800 wa maeneo hayo kutokana na shida kubwa ya maji iliyokuwa ikiwakabili kabla ya mradi huo kuanza.
Kutokana na kukamilika mradi huo, Manyaku alisema kuwa asilimia 85 ya wakazi wa maeneo hayo sasa watapata maji safi na salama.
Mara baada ya kuzindua mradi huo, Mtendaji Mkuu wa Shirika la MEDICOR la nchini Uingereza, Fortunat Walther, aliutaka uongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Iramba kuutunza, kuulinda na kuufanyia matengenenezo ya mara kwa mara mradi huo ili uweze kuwa endelevu.
Baadhi ya wakazi wa maeneo hayo walisema kuwa ujio wa mradi huo umekuwa ni ukombozi mkubwa kwao, hasa kwa akina mama waliokuwa wakitumia muda mwingi kufuata maji mtoni, ambayo hata hivyo hayakuwa safi wala salama.
“Kabla ya mradi huu, tulikuwa tunaamka alfajiri kwenda mtoni kufuata maji au wakati mwingine tulikuwa tunaletewa na tela na kuuziwa na wafanyabiashara hao kwa bei ya sh 300 kwa ndoo moja lakini sasa tunapata kwa sh 50 tu” alisema Amina Juma ambaye aliungwa mkono na Amina Mkoma.
Naye Juma Japhet alisema kuwa kabla ya  hapo akina mama walikuwa wanahangaika kufuata maji mbali hivyo kupoteza muda mwingi kusaka maji badala ya kutumia muda huo kufanya shughuli za maendeleo.


Related

TUTATUMIA NGUVU YA UMMA KUKWAMISHA KATIBA: CHADEMA

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema kitatumia nguvu ya umma kuikataa Katiba Mpya endapo CCM na Serikali yake: “vitaendeleza hila na ubabe katika mchakato unaoendelea.” Pia c...

VIJANA NCHINI KENYA WAWEZESHWA

Rais Kenyatta jana amezindua Uwezo Fund kuwasaidia vijana na wanawake nchini humo. Kiasi cha sh. 6 bilion za Kenya zimetengwa kuwakomboa kiuchumi, na rais amewataka vijana kujituma ili kufanikisha...

GHANA YAIBAMIZA ZAMBIA BAO 2 - 1

Ghana National Team Timu ya taifa ya Ghana imefanikiwa kuifunga timu ya taifa ya Zambia bao 2 - 1 katika mchezo uliochezwa leo kuwania kushiriki kombe la dunia 2014

Post a Comment

emo-but-icon
:noprob:
:smile:
:shy:
:trope:
:sneered:
:happy:
:escort:
:rapt:
:love:
:heart:
:angry:
:hate:
:sad:
:sigh:
:disappointed:
:cry:
:fear:
:surprise:
:unbelieve:
:shit:
:like:
:dislike:
:clap:
:cuff:
:fist:
:ok:
:file:
:link:
:place:
:contact:


LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

904754
item